Psalms 129
Choose a chapter
123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150
1Wimbo wa kwenda juu. Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa: 2wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda. 3Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu. 4Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu. 5Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu. 6Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua; 7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake. 8Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.”
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Open Kiswahili Contemporary Version) © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under CC BY-SA 4.0.