Psalms 67
Choose a chapter
123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150
1Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo. Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake, 2ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote. 3Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. 4Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia. 5Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. 6Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki. 7Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Open Kiswahili Contemporary Version) © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under CC BY-SA 4.0.