Psalms 87
Choose a chapter
123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150
1Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu; 2Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo. 3Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu: 4“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’” 5Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.” 6Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.” 7Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.”
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Open Kiswahili Contemporary Version) © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under CC BY-SA 4.0.